Mount Kilimanjaro

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

 
ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Majambazi wavamia benki ya NMB - Temeke

31/07/2009

Mkurugenzi wa Upeleleza wa Makosa ya Jinai afande Robert Manumba akiongea na waandishi wa habari nje ya benki ya NMB, Temeke, Dar es Salaam palipotokea tukio la kuvamiwa na majambazi. Waziri wa Mambo ya Ndani, Mh. Lawrence Masha, Mkuu wa Polisi IGP Saidi Mwema na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Mh. William Lukuvi pia walikuja eneo la tukio baadaye na kutembelea majeruhi waliolazwa hospitali ya Temeke iliyo jirani na Benki hiyo.

Pichani ni damu ya wafanyakazi wa katika kaunta ya benki ya NMB tawi la Temeke ambapo majambazi yapatayo saba hivi yalivamia kwa mabomu ya mkono ambapo baada ya kurusha mawili nje na kuua mlinzi wa kampuni binafsi aliyekuwa getini, yakarusha risasi ndani na kujeruhi watu 13, ikiwa ni pamoja na askari polisi wawili na kukomba takriban shilingi milioni 150 kabla ya kutoroka. Majambazi hao walitoroka na Escudo na Prado zilizokuwa na namba za 'SU' na 'STJ'.

Afande wa FFU akiwa na guruneti moja ambalo halikulipuka katika uporaji wa benki ya NMB tawi la Chang'ombe huko Temeke.

Wafanyakazi na wahusika mbalimbali wakipigwa na butwaa baada ya tukio hilo kutokea.

Hii si mara ya kwanza kutokea uporaji wa aina hii na umekuja siku moja tu baada ya Kamanda wa kanda maalumu ya Dar es Salaam, Afande Suleiman Kova kutoa tahadhari kwamba taarifa za kiintelejensia zao zinaonesha kuna kundi la majambazi yenye silaha kali linataka kufanya uhalifu jijini. Tukio kama hilo lilipata kutokea benki ya za Ubungo, Mwanga na Mbeya.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
News Archive

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©