Mount Kilimanjaro

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

 
ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Sh. Bilioni 230 msaada kutoka Uingereza

05/08/2009

Uingereza imeipatia Tanzania Sh. bilioni 230 kwa ajili ya kusaidia bajeti ya mwaka huu, huku ikiitaka ijidhatiti kupambana na rushwa.

Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza (DFID), Darren Welch, aliyasema hayo alipokutana na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, jijini Dar es Salaam.

Uingereza ndiye mshirika wa maendeleo iliyotoa fedha nyingi kulinganisha na nchi zingine. Jumla ya fedha zote zilizokwishatolewa na washirika wa maendeleo zinafikia Sh. bilioni 424.

Welch alisema Uingereza inatekeleza ahadi zake na imejikita kuisaidia Tanzania hata katika kipindi hiki kigumu cha mtikisiko wa fedha duniani. Alisema fedha hizo zimeingizwa kwenye bajeti ya serikali kwa mkupuo mmoja mwanzoni mwa mwaka huu wa fedha kulingana na mchakato wa bajeti ya serikali.

"Tunataka kuona watu wengi zaidi wakipata maji safi na salama, wanawake wengi zaidi wakijifungua salama na watoto wengi wakienda shule... Kwa hiyo tuko mstari wa mbele kuisaidia Tanzania katika harakati zake za kupunguza umaskini na kuboresha maisha ya watu wake," alisema. Alisema lazima serikali ijitahidi kuboresha mazingira ya biashara ili sekta hiyo ikue na na kuongeza ajira kwa wananchi.

Welch pia alitangaza kuzinduliwa kwa mkakati mpya wa serikali ya Uingereza unaohusu maendeleo ya kimataifa.

"Mkakati huu unasisitiza nia ya Uingereza kuendelea kuchangia maendeleo ya kimataifa hasa katika kipindi hiki kigumu cha msukosuko wa uchumi," alisema Welch.

Naye Waziri Mkulo alisema hatua ya wafadhili hao kuisaidia Tanzania ni ishara ya imani waliyo nayo kwa serikali ya Tanzania. Alisema Benki ya Dunia (WB) na Benki ya Maendeleo Afrika (ADB), tayari ziko katika mchakato wa kuisaidia serikali katika bajeti ya mwaka huu.

Alikiri kuwa kuna udhaifu katika mfumo wa malipo ya fedha za serikali lakini aliahidi kuwa serikali italifanyia kazi mfumo wa marekebisho ya usimamizi wa fedha wa Tanzania uwe imara zaidi.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
News Archive

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©