Mount Kilimanjaro

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

 
ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Serikali yaeleza chanzo cha Ujambazi hivi sasa Tanzania

08/08/2009

SERIKALI imesema kukithiri kwa matukio ya ujambazi nchini hivi sasa kunachangiwa na ongezeko la idadi ya watu linalokwenda sambamba na kasi ya maendeleo nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Bw. Lawrence Masha (pichani juu), alisema Serikali imejipanga kuhakikisha inakabiliana na kudhibiti uovu huo kwa gharama yoyote.

Alisema Tanzania sasa ina wastani wa watu milioni 40 ongezeko linalokwenda sambamba na maendeleo katika nyanja mbalimbali nchini jambo linalochangia kuongezeka vitendo vya uhalifu.

"Katika nchi kama hii yenye wastani wa watu milioni 40 kukithiri matukio ya ujambazi ni hali yenye kutarajiwa kadiri nchi inavyoendelea," alisema.

Alisema sababu nyingine ya kukithiri kwa matukio hayo ni Tanzania kupakana na nchi zenye machafuko yanayohusisha matumizi ya silaha za kivita hivyo kuna uwezekano mkubwa wa silaha hizo kuingizwa nchini kwa magendo na kutumika katika uhalifu.

Bw. Masha alikiri kuwa Serikali haina uwezo wa kukidhi vitendea kazi vya kudhibiti uhalifu hali inasababisha kutegemea misaada kutoka kwa wahisani mbalimbali.

Alisema Jeshi la Polisi litaongeza nguvu zake kwa kujenga ukaribu na raia na kuongeza idadi ya vituo kwa lengo la kuimarisha ulinzi shirikishi.

Alisema wizara yake imejipanga kuwasaka wahalifu wa ndani na nje ya nchi ili kuhakikisha amani na utulivu vinadumishwa nchini.

"Tumejipanga kusaka wahalifu Wakitanzania na wakigeni ili kuimarisha amani nchini kwani pande zote mbili zinaweza kuwa chanzo cha uhalifu hivyo hatuwezi kupuuzia upande mmoja, alisema Bw. Masha.

Alitoa mwito kwa wananchi kutoa taarifa zitakazosaidia kudhibiti na kukamatwa wahalifu katika matukio mbalimbali.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
News Archive

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©