UNHCR yatoa msaada kwa
Polisi
10/08/2009

Mwakilishi mkazi wa shirika
linaloshughulikia wakimbizi nchini (UNHCR) Bw. Yakoub El Hillo akikata
utepe kama ishara ya makabidhiano ya magari na pikipiki kwa jeshi la
polisi nchini ili kusaidia kupambana na uhalifu. Wanaoshuhudia kulia ni
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Rawlence Masha, kushoto ni Mkuu wa
jeshi la polisi nchini IGP Said Mwema na katikati ni Mkurugenzi wa
upelelezi wa makosa ya Jinai (DCI) Robert Manumba.

Makabidhiano hayo yamefanyika katika Makao
makuu ya Wizara ya Mambo ya ndani ambapo UNHCR imekabidhi magari aina ya
Toyota Prado 2, Toyota Hardtop 6 na pikipiki 10 vyote vikiwa na thamani
ya Dola za kimarekani 241,000.
|