Mount Kilimanjaro

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

 
ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Serikali haina mpango wa kuongeza bei ya umeme

14/08/2009

SERIKALI imesema hakuna mpango wa kupandisha bei ya umeme nchini kwa sasa. Akizungumza jijini Dar es Salaam juzi, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja alisema hakuna kampuni wala shirika lolote nchini, linaloweza kupandisha bei ya umeme bila kupata kibali cha serikali.

Hivi karibuni pamoja na kuwepo kwa sheria inayoruhusu kampuni mbalimbali binafsi pamoja na Shirika la Umeme nchini (Tanesco ) kutoa huduma ya umeme, lakini hazitakuwa na uwezo wa kupandisha bei bila idhini ya serikali.

“Hata Tanesco walitaka kupandisha bei ya umeme, lakini walizuiliwa na EWURA kwa kuwa wao ndio wasimamizi wa masuala hayo na ni chombo cha serikali,” alisema.

Ngeleja ambaye alikuwa akifungua mkutano wa Ushirikiano wa Miundombinu kwa ajili ya Maendeleo ya Afrika, (iPAD), alisema serikali inafanya kila jitihada kuhakikisha kuwa mlaji anapata umeme kwa bei nafuu, lakini akakumbusha wananchi kuwa umeme huo ni lazima ulipiwe ili kuweza kuusambaza zaidi nchini.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
News Archive

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©