WAMA yazawadiwa na UNICEF
16/08/2009

Mke wa Rais Mama Salma
Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA)
akiangalia zawadi ya kanga iliyoandikwa “Tuungane kwa ajili ya watoto”
aliyopewa na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
mambo ya watoto (UNICEF) Heimo Laakkonen.
Laakkonen pamoja na
Makamishina wenzake walitembelea ofisi za WAMA kwa ajili ya kutoa
mrejesho wa shughuli ya ziara yao ya wiki moja waliyoifanya hapa nchini
baada ya kupata mwaliko kutoka wizara ya Maendeleo ya jamii, jinsia na
watoto.
|