Kikwete azuru Longido na
afuturisha Arusha
24/08/2009

Rais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya
wazee wa kabila la Wamasai katika kijiji cha Engarenaibor, wilaya ya
Longido ambapo alikwenda kukagua hali ya ukame na upatikanaji wa chakula
cha msaada katika wilaya hiyo iliyoathirika vibaya kwa ukame. Katika
ziara hiyo Rais alitembelea pia kijiji cha Mundarara ambapo aliongea na
wananchi baada ya kupata taarifa ya hali ya ukame katika makao makuu ya
wilaya mpya ya Longido na usiku kuelekea Arusha mjini kwa mwaliko wa
kufuturisha katika mwezi mtukufu wa Ramadhan.

JK akitoa zawadi kwa
baadhi ya wageni walioshiriki katika futari aliyoiandaa Ikulu ndogo
mjini Arusha jioni baada ya kurejea toka Longido.

Mama Salma Kikwete
akisalimiana baadhi ya wageni walioshiriki katika futari waliyoiandaa
Ikulu ndogo mjini Arusha.
|