Jeshi la Wananchi Tanzania
(JWTZ) kuadhimisha miaka 45
30/08/2009

Mkuu wa Majeshi Jenerali
Davis Mwamunyange akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya
mambo ya nje Ulinzi na Usalama bwana Wilson Masilingi mara baada ya
ufunguzi wa maadhimisho ya JWTZ kutimiza miaka 45. Mh. Masilingi alikuwa
mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa Maadhimisho hayo yaliyokuwa katika kikosi
cha 603 cha jeshi eneo la Airwing, Ukonga jijini Dar es salaam. Kulia ni
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dk. Hussein Mwinyi na wa
kwanza kushoto ni Naibu wake Dk. Emannuel Nchimbi.

Baadhi ya wananchi
wakijitokeza kuangalia maonesho ya wiki ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania
(JWTZ) kutimiza miaka 45 wakipata maelezo kuhusu silaha za kivita kutoka
kwa wataalam wa Jeshi hilo.

Mwenyekiti wa Kamati ya
Bunge ya mambo ya nje, Ulinzi na Usalama Mh. Wilson Masilingi akipata
ufafanuzi kutoka kwa Luten Kanali Anselum Bahati kuhusu bidhaa
mbalimbali zinazotengenezwa na JWTZ kikosi cha Nyumbu wakati wa maonesho
ya miaka 45 ya JWTZ. Kushoto ni Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis
Mwamunyange.

Wananchi wakijitokeza
katika mabanda ya huduma za tiba kwenye maonyesho ya Jeshi la Wananchi
wa Tanzania kutimiza miaka 45.

Baadhi ya wananchi
waliojitokeza kwenye maonyesho ya JWTZ kutimiza miaka 45 wakipata huduma
za tiba na ushauri katika mabanda ya Maonyesho katika viwanja vya kikosi
cha 603 cha Jeshi la Wananchi, Air wing, Ukonga jijini Dar es salaam.

Mkuu wa Majeshi Jenerali
Davis Mwamunyange na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya mambo ya nje
Ulinzi na Usalama bwana Wilson Masilingi wakipata maelezo mara baada ya
ufunguzi wa maonesho na maadhimisho ya JWTZ kutimiza miaka 45. Mh.
Masilingi alikuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa Maadhimisho hayo
yanayoendelea katika kikosi cha 603 cha jeshi eneo la Airwing, Ukonga
jijini Dar es Salaam.

Askari wa kikosi cha anga
katika maonesho hayo, wakiwakilisha kitengo chao cha anga huku kushoto
ikionekana nembo yao ambayo imeandikwa UMOJA.

Wanafunzi wakiangalia
baadhi ya silaha katika maonesho hayo.

Askari wenye silaha zenye
nguvu za kutungua ndege katika maonesho.

Wananchi wakiangalia vifaa
vya kijeshi kwenye maonesho hayo yaliyofanyika Air Wing, Ukonga mjini
Dar es Salaam.
|