Mount Kilimanjaro

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

 
ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

MV Magogoni mzigoni

01/09/2009

Kivuko cha MV Magogoni kilichoundwa hapa Dar es Salaam kwa gharama ya Sh 8.5 bilioni na chenye uwezo wa kubeba tani 500 wakiwemo abiria 2,000 na magari 60 kimeleta wepesi kwa abiri wanaotumia kivuko hicho katika misafara yao ya kila siku kivukoni.

Sehemu ya juu ya abiria inavyoonekana kabla hawajaingia ndani.

Sehemu inayopakia magari ikionekana imebeba magari na baadhi ya sehemu zikionekana bado ziko wazi.

Sehemu ya abiria ikionekana imechukua watu kwa tanafasi na si kama ilivyokuwa zamani kubanana kama mshikaki. Kwa mbaali kulia MV Alina ikionekana bado ikipiga mzigo kama kawaida.

MV Magogoni ikielekea Kigamboni.

MV Magogoni ikikata maji kutoka Kigamboni. Usafiri wa kivukoni umekuwa si wa shida tena kutokana na ujio wa MV Magogoni toka rais JK kuzindua rasmi kivuko hicho mwezi Juni mwaka huu na mchango mkubwa wa MV Alina kufanya kazi katika kivuko hicho.

MV Alina ikionekana inapiga mzigo kama kawaida. Hali hii imesaidia kupunguza ajali ambazo zilikuwa zikitokea mara kwa mara hapo awali katika kivuko hicho.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
News Archive

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©