Roman Abromavich atembelea
Tanzania
02/09/2009

Bilionea na mwenye kumiliki timu ya
Chelsea ya England bwana Roman Abromavich ametua kiwanja cha ndege cha
Kilimanjaro Internationa Airport katika ziara yake ya kutembelea mbuga
za wanyama na mlima wa Kilimanjaro.

Mara baada ya kutua uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Kiliimanjaro, bilionea huyo alielekea moja kwa moja katika
hoteli inayojulikana ya hali ya juu Grumeti Luxury Lodge iliyopo
Serengeti National Park. Abromavich hajajulikana safari yake ni ya siku
ngapi nchini.
|