Yanga (Dar Young Africans)
04/09/2009

Klabu ya
timu ya vijana wa mjini Dar es Salaam (Dar Young Africans) ijulikanayo
kwa jina maarufu 'Yanga' ambayo ipo katika viwanja vya Jangwani, ipo
katika ukarabati wa nguvu wa kuirudisha klabu hiyo katika hali yake
iliyokuwa, ikiwa kama ni timu kubwa moja wapo ya timu za kitaifa za
Tanzania ikiwamo timu ya Simba na nyinginezo.

Katibu
mkuu mpya wa kuajiriwa wa Yanga, bwana Lawrence Mwalusako (shoto) akiwa
na aliyekuwa katibu mkuu wa klabu hiyo bwana Lucas Kisasa, wakati
Mwalusako alipowasili Jangwani kuanza kazi rasmi.

Lawrence
Mwalusako akiongea na mshambuliaji Mrisho Ngasa anayepiga tizi kwenye
gym ya Yanga iliyo katika klabu hiyo mtaa wa Twiga, Jangwani mjini Dar
es Salaam.
|