Mandy Juma apewa fursa
kuendeleza kipaji cha Tennis
12/09/2009

Kijana
Mandy akijidai na bendera ya taifa akiwa ubalozini jiini London
alipofika kumsalimia Balozi wetu Uingereza Mh. Mwanaidi Maajar.

Mheshimiwa Mwanaidi Maajar akiwa na kijana
Mandy ubalozini London.

Mandy
akiwa pamoja na Baba yake Bwana Juma Rajabu Furaji na Bwana Hareen
Wasantha, Mkurugenzi na ni Kocha wake.

Mandy
akiwa kwenye picha ya pamoja na Mh. Balozi, wenyeji wake, baba mzazi,
Kocha na Maofisa wa Ubalozini.
Mandy
Juma Rajabu Furaji ni kijana mdogo wa Kitanzania aliyebahatika kupata
ufadhili wa kuhudhuria chuo maalum cha kufundishia mchezo wa Tennis
kiitwacho Tennis Avenue Academy hapa nchini Uingereza.
Kijana
Mandy akiongozana na baba yake Bwana Juma Rajabu Furaji na wenyeji wao
hapa Uingereza, Bwana na Bibi Mansela, walipata nafasi ya kutembelea
Ofisi za Ubalozi wa Tanzania hapa nchini Uingereza, na kupokewa na
Mheshimiwa Balozi, Mwanaidi Senare Maajar, pamoja na maofisa wengine wa
Ubalozini hapo.
Baada ya
kufanyiwa majaribio kadhaa na Walimu na Wataalamu wa Chuo hiko
wamefurahishwa na wameridhia na kipaji, kiwango na umakini wa kijana
Mandy na kumzawadia Scholarship (Ufadhili) kwa Umahili wake alionao
kwenye mchezo huo maarufu wa Tennis.
Ikumbukwe kuwa mchezo huo wa Tennis ni ghali sana nchini Uingereza na
kwenye nchi zilizoendelea. Mandy ataendelea na mafunzo yake ya Tennis
chini ya Kocha wake na ambaye ni Mkurugenzi wa chuo hiko cha Tennis
Avenue Academy kilichopo maeneo ya New Malden Surrey, Bwana Hareen
Wasantha.
|