Salaam za Eid Mubarak
kutoka kwa Balozi wa Tanzania
18/09/2009

Ninayo furaha kubwa kuwatumia Mkono wa Idd...
, mwaka huu wa 2009. Kwa niaba ya Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kwa niaba ya wafanyakazi wenzangu
katika Ubalozi wa Tanzania London, na kwa niaba yangu binafsi, napenda
kuchukua fursa hii kuwapongeza kwa kumaliza salama mfungo wa mwezi
Mtukufu wa Ramadhani. Nawatakieni nyote kila la kheri wakati huu wa
sikukuuu.
Idd Mubarak.
Mheshimiwa Balozi wa Tanzania nchini UK,
Mwanaidi Sinare Maajar.
|