Kombe la Dunia kufanya
ziara Tanzania
23/09/2009

Kombe la Dunia ambalo
litafanya ziara nchini Tanzania mwezi wa Novemba mwaka huu kwa hisani ya
kampuni ya Coca Cola, litaanikwa katika uwanja mpya wa Taifa uliopo
jijini Dar es Salaam. Ziara yake
hiyo pia itatumika kunadi uwanja huo mpya wa taifa nchini Tanzania kuvutia
timu zitakazo shiriki kwenye shindano la Kombe la Dunia 2010 wafanyie
mazoezi kwa makubaliano maalum.
Mashindano hayo ya kombe la Dunia
yanatarajiwa kuwa mwakani (2010) wakati wa kiangazi nchini Afrika ya
Kusini (South Africa).
|