GORDON BROWN atunukiwa "World
Statesman of the Year 2009"
25/09/2009

WAKATI Waziri Mkuu wa United Kingdom bwana
Gordon Brown (pichani kushoto) akisubiri uchaguzi mkuu mwakani na huku
akijaribu kuthibitisha kwa wananchi wake kuleta maendeleo ya huduma
nzuri na hali bora kwa wananchi katika hali ngumu ya kiuchumi duniani,
bwana Gordon Brown alipatiwa sifa kemkem na viongozi wakubwa kutoka
madola mengi duniani kwa mtazamo wake wa mfumo wa kiuchumi ambao
ameupendekeza na kutumiwa ambao unatarajiwa kuleta mabadiliko makubwa ya
mfumo wa kifedha duniani ambao utasaidia miaka ijayo kuweka uchumi wa
kidunia katika hali nzuri.
Ingawa bwana Gordon Brown anapewa mitihani
na viongozi wa vyama vingine vya kisiasa nchini UK na kumfanya kazi yake
kubwa aliyoifanya ya kuwezesha kurejesha uchumi isivume sana nchini UK,
lakini amewika duniani kote nje ya UK na viongozi wa madola wamempa sifa
kwa kipaji alichokuwa nacho cha kuweza kuufuma upya mfumo wa kifedha wa
kiuchumi wa dunia nzima na kuutokomeza mfumo uliokuwepo mwanzo ambao
ulisababisha kuanguka kwa uchumi hivi karibuni.

Baadhi ya viongozi waliompa sifa hizo
akiwamo Queen Rania wa Jordan, mkewe mfalme wa Jordan King Abdallah,
muimbaji maarufu wa nchi za Ulaya na Marekani, bwana Bono, bwana Henry
Kissinger, aliyekuwa Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, rais Barack
Obama wa Marekani na wengi ambao wameona mfumo huo wa kifedha utasaidia
kuwezesha kutoka katika hali ngumu ya kiuchumi iliyopo hivi sasa.
Nchini Marekani bwana Gordon Brown amewika
vikali na kuzawadiwa rasmi zawadi kubwa ambayo hutolewa kwa viongozi
maalum wenye kuleta mabadiliko maalum katika mwaka maalum, ambayo
alizawadiwa bwana Gordon Brown "World Stateman of the Year 2009" kwa
kuleta mabadiliko ya mfumo mpya wa kiuchumi duniani.
Mtazamo huu ndio uliomfanya rais wa
Marekani Barack Obama alipoulizwa na waandishi wa habari kuwa ni kitu
gani kitamfanya bwana Gordon Brown kushinda uchaguzi mwakani, Obama
alisema "whatever the problems faced, good policy would win out over
time".
|