Mount Kilimanjaro

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

 
ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Wanafunzi wajawazito mikoa ya Pwani na Visiwani inazidi

06/10/2009

Jumla ya wanafunzi 287 wamepata ujauzito kwa kipindi cha miezi tisa katika mkoa wa Pwani na hivyo kushindwa kumaliza elimu ya msingi na sekondari.

Hayo yamesemwa jana na Mkuu wa Mkoa huo Hajati Amina Mrisho Said wakati akisoma taarifa ya maendeleo ya mkoa kwa mke wa Rais Mama Salma Kikwete aliyetembelea shule ya Sekondari Magindu iliyopo wilayani Kibaha kwa ajili ya kutoa msaada wa magodoro 100 na vitanda vyake.

Hajati Amina alisema kuwa wilaya ya Rufiji inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi waliopata ujauzito kwani kuanzia Januari hadi Septemba mwaka huu wanafunzi 130 wamepata ujauzito ambapo wanafunzi wa Shule ya Msingi ni 110 na Sekondari ni 20. Aliitaja wilaya ya Mafia kuwa haina tatizo kubwa la wanafunzi kupata ujauzito ukilinganisha na wilaya zingine kwani kwa mwaka huu wanafunzi wa shule ya Msingi watatu na sekondari kumi ndio waliopata ujauzito.

Hali kama hiyo imeikumba visiwa vya Zanzibar kutokana na takwimu na ripoti za serikali. Kwani ni muhimu suala hili kuangaliwa na kufanyiwa uchunguzi wa karibu kabisa ili kuainisha ni vitu gani vinavyoendesha watoto hao kufikia kupata mimba hali ya kuwa bado wapo masomoni na kwanini ukanda wa mikoa ya pwani ambayo ina takwimu kubwa za kustusha kama hivi!?

Kwa maelezo zaidi ya takwimu za Zanzibar kuhusu hali hii na utaratibu uliochukuliwa, bonyeza hapa.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
News Archive

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©