Cheti kipya cha kuzaliwa -
Tanzania
21/10/2009

SERIKALI imebaini kuwa zaidi ya asilimia
90 ya wananchi wanaoishi katika mikoa ambayo iko karibu na nchi jirani
wanatumia vyeti vya kughushi kwa ajili ya shughuli zao mbalimbali.
Utafiti huo ambao umefanywa na vyombo mbalimbali kwa kushirikiana na
Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) ambapo wamebaini kuwa,
wananchi hao wameghushi vyeti hivyo kwa ajili ya kupata hati ya kuzaliwa
na vifo.
Akizungumza katika uzinduzi wa cheti kipya cha kuzaliwa chenye alama za
usalama, uliofanyika jijini Dar es Salaam jana, Waziri wa Katiba na
Sheria, Mathias Chikawe alisema kuuwa, kutokana na hali hiyo serikali
imejidhatiti kudhibiti hali hiyo.
Alisema mpaka sasa idadi ya watu wanaoishi na vyeti hivyo ni wengi,
jambo ambalo linaonyesha wazi kuwa wanakiuka sheria na taratibu za
upatikanaji wa vyeti halali, kutokana na hali hiyo,wameandaa mkakati wa
kuzunguka nchi nzima kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi juu ya
madhara ya matumizi ya vyeti bandia na kuwataka watafute vyeti halali
kwa ajili ya shughuli zao.
“Tunajua kama kuna baadhi ya watu wanatumia vyeti bandia kwa ajili ya
shughuli zao,ambavyo wamevipata kwa njia isiyo halali jambo ambalo
linaonyesha wazi kuwa wanavunja sheria,kutokana na hali hiyo tumeamua
kubadilisha mfumo wa vyeti vya zamani na kutengeneza vya kisasa ambavyo
vitatumia teknolojia na kompyuta ili kuwadhibiti watu wanaovighushi,”
alisema Chikawe.
Aliongeza kuwa kutokana na hali hiyo vyeti vya zamani vitaendelea
kutumika mpaka hapo watapopitisha sheria ya kuvibadilisha ili kila mmoja
aweze kuwa na vyeti vya kisasa ambavyo ni vigumu kwa mwananchi wa
kawaida kuvitengeneza.
Alisema kutokana na hali hiyo wananchi wenye tabia ya kughushi vyeti
hiyo wametakiwa kuacha mara moja kwa sababu ni kos ala jinai ikiwa mtu
atabainika maehusika katika zoezi zima la kughushi vyeti hivyo na
kuchukulia hatua kaliza kisheria.
Naye Kaimu Mtendaji Mkuu wa RITA, Philip Saliboko alisema kuwa vyeti
hivyo vipya vitaanza kutolewa leo katika ofisi za RITA zilizopo Upanga
jijini Dar es Salaam.
|