Mount Kilimanjaro

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

 
ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Kesi ya Liyumba kuanza upya

22/10/2009

ALIYEKUWA Mkurugenzi wa utumishi na utawala wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Amatus Liyumba (pichani),ambaye anakabiliwa na tuhuma za kutumia madaraka vibaya na kuisababishi Serikali hasala ya mabilioni, ndiye aliyekuwa akiagiza kufanyika kwa mabadiliko katika ujenzi wa majengo ya benki hiyo, yaliyoisababishia Serikali kupata hasara.

Hayo yalielezwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, na shahidi wa kwanza kutoka katika upande wa mashitaka wa kesi hiyo, ambayo Liyumba nadaiwa kuisababishia Serikali hasara ya Sh Bilioni 221, kupitia ujenzi wa majengo pacha ya BoT.

Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Edson Mkasimongwa, shahidi huyo Seif Mohamed ambaye ni mchunguzi kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), alidai mahakamani hapo kuwa Liyumba ndiye aliyekuwa na jukumu la kusimamia ujenzi wa jingo hilo.

Akiongozwa na Wakili wa Serikari Juma Ramadhani, Mohamed alidai kuwa Liyumba alikuwa akitoa maagizo ya kwa aliyekuwa msimamizi wa wakandarasi mkuu wa jengo hilo, juu ya mabadiliko ya jingo bila kupitia kwa bodi ya benki hiyo.

Alidai kuwa Mkuu huyo wa wakandarasi, alikuwa akikubaliana na mabadiliko hayo, na kuidhinisha kufanyika katika jingo, jambo ambalo ni kinyume na makubaliano ya mkataba kati ya benki hiyo na kampuni ya ujenzi wa jengo hilo.

Shahidi huyo alidai kuwa baadhi ya mabadiliko ambayo Liyumba aliyafanya, yalisababisha gharama ya jingo hilo kufikia Dola za Marekani Milioni 357.7, badala ya kiwango kilichoidhinishwa hapo awali cha Dola za Marekani Milioni 73.6.

Aliongeza kuwa katika mkataba ambao BoT iliingia na kampuni ya ujenzi wa jengo hilo, bodi ya ya benki hiyo ilidhinisha gharama hizo za awali kwasabau iliamini kuwa zingetosha kufanyika kwa ujenzi huo.

Kwa mujibu wa shahidi huyo, Liyumba alikuwa akipeleka mapendekezo ya mabadiliko hayo kwa bodi ya benki hiyo, baada ya kuwa mabadiliko kutendeka.

Naye Wakili Hillary Mkate ambaye anamtetea mshitakiwa huyo, alimuuliza shahidi huyo maswali, ambapo Maojiano yao yalikuwa kama ifuatavyo;

Mkate: maelezo ya mwanzo yalidai kuwa bodi ya BoT iliruhusu mabadiliko hayo kufanyika, je wewe unasemaje juu ya hilo?

Shahidi:hapana Liyumba alikuwa anatoa maagizo, ya mabadiliko na kabla hata ya bodi kuidhinisha na mabadiliko yalikuwa yakifanywa.

Mkate:ni nani ambaye anamamlaka ya kubadili makubaliano yaliyokubaliwa katika mkata?

Shahidi:ni bodi ya benki ndiyo iliyokuwa na uwezo huo, ingawa haikuhusika katika mabadiliko hayo yaliyoisababishia Serikali hasara

Mkate:Imekuwaje Liyumba afanye mabadiliko hayo yanayohusisha mabilioni ya fedha, bila kuihusisha bodi iliyokuwa na mamlaka ya kutoa fedha, wakati yeye alikuwa si mjumbe wa bodi?

Shahidi:Liyumba alikuwa akiidhinisha kwanza mabadiko, kisha alikuwa akirudi kwa bodi na kupeleka taarifa hiyo.

Mkatel:Na bodi hiyo ilikuwa ikisema nini juu ya hilo...???

Shahidi:Mara kadhaa bodi ilikuwa ikimkanya Liyumba kutokana na suala hilo lakini aliendelea kufanya maamuzi bila kuishirikisha bodi.

Wakili Mkate aliendelea kuhoji suala hilo, huku akidai kuwa iweje bodi hiyo ikubaliane na tabia ya Liyumba ya kufanya mabadiliko bila kuishirikisha, na isimchukulie hatua?

Shahidi huyo alionekana kutokuwa na majibu ya maswali hayo.

Kesi hiyo iliahirishwa hadi leo, ambapo mahakama hiyo itasikiliza ushahidi wa shahidi wa pili katika kesi hiyo.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
News Archive

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©