Ujenzi wa barabara wapata
msaada kutoka Abu Dhabi
29/10/2009

Balozi wa Tanzania nchini UAE, Mhe.
Mohamed Maharage Juma (kulia) akiwa na muwakilishi wa Mwendeshaji wa
Utendaji kazi wa mfuko wa usaidizi wa Abu Dhabi (Abu Dhabi Fund) bwana
Mohamed Saif Al Suwaidi, katika kuwafiki makubaliano ya kipesa ya ujenzi
wa barabara baadhi ya sehemu za nchini Tanzania.
Makubaliano hayo yalifanyika katika makao
makuu ya Abu Dhabi Fund iliyopo mjini Abu Dhabi, UAE, ambayo
yanatarajiwa kuendesha ujenzi wa barabara ya Kidahwe-Uvinza, ambayo ina
umbaliwa kilomita 77.
Msaada huo umewafikiwa kwa kiasi cha dola
za Kimarekani $57,200,000 ikiwamo $11,084,108 za gharama za mradi maalum
ulioghairishwa mwaka 1976 wa mitambo ya sukari ya Kagera.
|