Mount Kilimanjaro

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

 
ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Waziri Aisha ataka orodha ya mabosi waombao ngono kwa kutoa ajira

01/11/2009

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imewataka wanawake wenye kuombwa ngono ya mapenzi wakati wanapotafuta ajira sehemu za kazi watumie simu zao za mkononi kuwarekodi watu wenye tabia hiyo ili kupata ushahidi wa madai hayo.

Waziri wa Kazi, Maendeleo ya Vijana, Wanawake na Watoto, Asha Abdallah Juma aliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi jana wakati  akijibu maswali mbalimbali katika kikao cha baraza la wawakilishi kinachoendelea Maisara Mjini Unguja.

Wanaodaiwa ngono ya mapenzi waseme na wasikae kimya na siku hizi mambo yameendelea, wanazo simu za mkononi, tunawaambia wanawake wenye simu watege sauti wanapotakiwa kimapenzi ni kunasa sauti za watu wenye tabia hiyo angalau mtu aje na ushahidi wa anayoyasema alisema Waziri huyo.

Alisema wizara yake inaendelea na usimamizi wa sheria ambapo ina jukumu kubwa ya kusuluhisha migogoro hiyo ya wafanyakazi kwa kuwarejesha kazini wale wote ambao wamefukuzwa kinyume cha sheria au kupatiwa maslahi yao ya kazi.

Wizara kwa nyakati tofauti inawaita ofisini mameneja na maafisa wanaotuhumiwa kuwalazimisha kingono wafanyakazi hao, inawaonya, baadhi yao wamechukuliwa hatua za kinidhamu na waajiri wao baada ya hatua yetu ikiwemo kuonywa vikali wengine kufukuzwa kazi na wengine kuondoshwa nchini alisema Waziri huyo.

Waziri huyo alisema katika matatizo yote hayo ya kufukuzwa kazi kwa wafanyakazi wa mahoteli hakuna malalamiko yanayotokana na mahusiano ya kimapenzi.

Malalamiko hayo yote yameshughulikiwa na Wizara yangu na wadai 29 wamelipwa haki zao ikiwemo dai moja ambapo mfanyakazi alirejeshwa kazini. Madai na malalamiko 10 yanaendelea kushughulikiwa alisema Waziri Asha.

Awali akijibu swali la msingi aliloulizwa na Mwakilishi wa Jimbo la Amani (CCM) Ali Denge Makame aliyetaka kujua kama wizara inafahamu tatizo la wafanyakazi kufukuzwa kazini bila ya utaratibu na baadhi yao kutakiwa kimapenzi na mabosi wao.

Waziri Asha alisema serikali inafahamu suala hilo na ndio maana inachukua hatua madhubuti ili kuweza kukabiliana na tatizo hilo ikiwa pamoja na kushughulikia malalamiko ya wafanyakazi wanaofukuzwa kazi bila ya kufuata utaratibu wa kazi kama unavyoelekeza.

Alisema kumekuwepo na manung'uniko na malalamiko ambayo baadhi yake yamewasilishwa wizarani kutoka kwa baadhi ya waafanyakazi wa mahoteli kwamba wanafukuzwa kazi na waajiri wao bila ya taratibu za kisheria kufuatwa.

Alisema katika kipindi cha januari hadi octoba mwaka huu wizara ya hiyo imepokea jumla ya madai na malalamiko 39 ya kufukuzwa kazi kwa Unguja na Pemba ambapo hakuna madai ya maandishi yaliowasilishwa yanayohusu kulazimishwa kingono na mabosi wao.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
News Archive

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©