Maisha Club yateketea
08/11/2009

Askari wa zimamoto
wakipambana na moto uliokuwa unateketeza jengo la Maisha Club ya
Oysterbay jijini Dar es Salaam. Hakuna aliyedhurika na janga hilo ambalo
chanzo chake bado haijajulikana wakati huo huo, japo redio mbao zimetaja
hitilafu zilizotokana na umeme.
Jengo hilo linalomilikiwa na Jenti Ladwa
na kukodishwa na Mfanyabiashara Hellen Sweya ambaye ndio mmiliki wa
klabu hiyo liliteketea kabisa kwa moto huo.
|