Mount Kilimanjaro

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

 
ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Mkutano wa kimataifa miaka 10 tangu Mwalimu kufariki

09/11/2009

Rais Mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi akiwasili Edinburgh, United Kingdom, kuhudhuria International High Level Conference on Nyerere. Mkutano huo unatarajiwa kuwa wa siku mbili ambao utazungumzia maisha ya Mwalimu Nyerere, mchango wake katika kujenga nchi na mpaka kifo chake mwaka 1999. Mkutano huo unafanyika katika chuo kikuu cha Edinburgh, Scotland, chuo ambacho alichosoma Mwalimu Nyerere kabla ya kuwa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Balozi wa Tanzania nchini Uingereza (UK) Mheshimiwa Mwanaidi Maajar (kushoto) akibadilishana mawazo na baadhi ya wageni waliohudhuria mkutano huo mjini Edinburgh, Scotland.

Waziri wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa, Mheshimiwa Bernard Membe (wa tatu Kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wageni waliohudhuria mkutano huo wa kutoka sehemu mbalimbali; wa kwanza kulia ni Mheshimiwa Mwanaidi Maajar. Mheshimiwa Bernard Membe alimwakilisha rais Kikwete katika mkutano huo.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
News Archive

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©