Pongezi kwa Rais Karume na
Maalim Seif
10/11/2009

Jumuiya ya Wazanzibari waishio
Uingereza (ZAWA-UK) inawapongeza Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Amani Abeid
Karume na Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Shariff Hamad kwa kukutana na
kuazimia kuwaunganisha Wazanzibari ili kuhakikisha kuwa Visiwa vya
Zanzibar vinakuwa na amani, mshikamano na kufungua milango zaidi ya
maendeleo. Hatua hii waliyoichukua tunaamini itafungua ukarasa mpya
katika siasa za Zanzibar.
Ahsante,
Abdulla A. Abdulla
Mwenyekiti, ZAWA, UK
|