Mafuriko Morogoro
14/11/2009

Gari la
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Issa Machibya, likipita katika dimbwi kubwa la
maji, katika barabara ya kwenda Kitongoji cha Mapangano, Kata ya Kanga,
Wilaya ya Mvomero, ambapo msitu wa hifadhi wa asili wa jumuiya ya Wami –
Mbiki ambapo wananchi wamevamia na kuweka makazi ya kudumu, kilimo
pamoja na wafugaji kuligeuza eneo la malisho ya mifugo.

Mkuu wa
Wilaya ya Kilosa, Halima Dendego ( kushoto) akiwa na Msaidizi wa Mkuu wa
Mkoa wa Morogoro, Ahmed Ng’eni, (kulia) wakipita kuangalia maeneo
yaliyokumbwa na mafuriko mjini Kilosa baada ya mto Mkondoa kuacha mkondo
wake wa maji na kusababisha kusambaa maeneo ya makazi ya wananchi na
shule ya msingi ya Mkondoa.

Duka la
Dawa muhimu ambalo linafanya kazi ya kutoa huduma kwa wananchi wa
kitongoji cha Mapangano, Kata ya Kanga, Wilaya ya Mvomero.
|