Waziri Batilda atembelea
kiwanda cha Bakhresa
05/12/2009

Pichani kushoto ni Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Dk. Batilda Burian akionyeshwa chembe
chembe za chupa zilizosagwa katika mtambo maalum na Meneja Mitambo Bw
Jones Solomon alipotembelea kiwanda cha kusaga taka za chupa cha Kampuni
ya Bakhresa kilichopo Chang'ombe jijini Dar es Salaam.

Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Dk. Batilda S. Burian ametembelea
Kiwanda cha kurejeleza (recycle) chupa za plastiki cha Bakharesa
kilichopo Chang’ombe jijini Dar es Salaam.
Mh. Dk.
Batilda amesema amefarijika kuona kuwa sasa kuna Kiwanda cha kurejeleza
chupa ambazo zilikuwa uchafu na kero katika Miji hususan jijini Dar es
Salaam.
Mhe. Dkt. Batilda amepongeza Kampuni ya Bakhresa kwa ukusanyaji chupa na
kuzirejeza. Amesema kuwa urejelezaji wa chupa hizi utasaidia katika
kupambana na uchafuzi wa mazingira na kusaidia kuwapa kipato wauzaji wa
chupa za plastiki zilizotumika.
Alisema chupa nyingi zinazoletwa ni chafu kwa hiyo zinahitaji kusafishwa
katika mtambo maalum uliopo kiwandani ambapo bidhaa inayozalishwa huwa
salama. Mhe. Dk. Batilda amesema Serikali tutaendelea kuhimiza utengaji
wa taka hivyo kuweza kurahisisha urejelezaji.
Mhe. Dk. Batilda alisema kuwa Ofisi yake itahahakikisha kuwa
vinaanzishwa vituo vya kukusanya chuo hizo na kuleta Kiwandani na
watalipwa pesa zao.
|