Mount Kilimanjaro

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

 
ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Wawili wapata tiketi ya mkutano wa 'Climate Change'

06/12/2009

Pichani kushoto ni Balozi wa UK nchini Tanzania, Diane Corner, akimkabidhi bwana Lucas Liganga mfano wa tiketi ya kwenda Copenhagen kwenye mkutano wa 'Climate Change'. Tiketi hiyo imetolewa baada ya wishindi hao kushida katika mashindano maalum ya uandishi ambayo washiriki mbalimbali walijihusisha kuandika athari za 'Climate Change'.

Pichani kulia ni Balozi wa UK nchini Tanzania, Diane Corner, akimkabidhi bwana Timothy Kitundu mfano wa tiketi ya kwenda Copenhagen kwenye mkutano wa 'Climate Change'. Tiketi hiyo imetolewa baada ya wishindi hao kushida katika mashindano maalum ya uandishi ambayo washiriki mbalimbali walijihusisha kuandika athari za 'Climate Change'.

Washindi hao wameshinda tiketi hizo za kuhudhuria mkutano wa Climate Change Conference (COP15) mjini Copenhagen mwaka huu. Bwana Liganga aliingia katika mashindano hayo na maandishi aliyoyaita "Climate Change: Over One million Tanzanians are at Risk of Starvation, Crops are Failing".

Na bwana Kitundu aliingia katika mashindano hayo na maandishi aliyoyaita "Climate Change Impact in Tanzania: Severe Strees in Social Structure". Mwingine ambaye alikuwa ni mshindi wa mwisho lakini hakupata nafasi ya tiketi bi Sharifa Kalokola aliingia na maandishi aliyoyaita "As Temperatures Rise, Malaria Deaths Soar".

Balozi Diane amesema, ameona ni muhimu matatizo ya Tanzania yahudhuriwe na yaelezwe na Watanzania wenyewe na Ubalozi huo umefurahi kudhamini mashindano hayo.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
News Archive

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©