Raia wa Congo wakamatwa
kwa kuishi bila
ya kibali
08/12/2009

Raia 10 wa Congo DRC
wakisubiri kupandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi wa
Sumbawanga baada ya kukamatwa kwa kosa la kuingia na kuishi nchini bila
kibali. Wanane kati yao walipewa adhabu ya kutumikia kifungo cha mwaka
mmoja jela baada ya kushindwa kulipa faini ya shilingi 30,000/- ambapo
wawili waliolipa faini hiyo walipewa masaa 72 wawe wamekwisha ondoka
nchini wenyewe kwa gharama yao.
|