Mount Kilimanjaro

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

 
ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Sherehe za Uhuru zaendelea Ikulu

10/12/2009

Rais JK akiongea na Mzee Rashid Mfaume Kawawa katika viwanja vya ikulu jana usiku wakati wa hafla maalum ya kusherehekea miaka 48 ya Uhuru.

Rais Jakaya Kikwete amesamehe wafungwa 4,135 kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 48 ya Uhuru wa Tanzania Bara.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na kusainiwa na Laurence Masha, imeeleza wafungwa walionufaika na msamaha huo ni ambao wanaotumikia kifungo kisichozidi miaka mitano na ambao hadi jana walikuwa wametumikia robo ya vifungo vyao.

Masha kupitia taarifa hiyo, alisema msamaha huo, aliotoa rais kwa mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa Ibara ya 45(1)(d) ya Katiba ya nchi na kwamba unawahusu pia wafungwa wenye ugonjwa wa ukimwi, Kifua Kikuu na saratani ambao hali zao siyo nzuri kiafya.

"Wafungwa hao, watathibitishwa na jopo la waganga chini ya uenyekiti wa Mganga Mkuu wa mkoa au wilaya," alisema Masha kupitia taarifa hiyo.

Taarifa hiyo, imeelez kuwa msamaha huo, unaotolewa karibu kila mwaka Desemba 9, utawahusu pia wazee wenye umri wa miaka 70 au zaidi, ambao umri wao utathibitishwa na jopo la waganga chini ya uenyekiti wa Mganga Mkuu wa mkoa au Wilya, wafungwa wa kike waliofungwa wakiwa wajawazito na walioingia gerezani na watoto wachanga.

Wafungwa wengine waliosamehewa ni wale wenye ulemavu wa mwili na akili, ambao ulemavu wao utathibitishwa na jipo la waganga chini ya uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa ya Wilaya.

Msamaha huo, hauwalengi wafungwa waliohukumiwa kunyongwa na kifungo cha maisha.

"Msamaha huo, pia hauwahusu wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa ya kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya, makosa ya rushwa, unyang'anyi wa kutumia silaha na wafungwa waliopatikana na hatia katika makosa ya kupatikana na risasi na silaha.

"Wafungwa wengine ambao hawamo katika msamaha huo ni waliohukumiwa kwa makosa ya kujamiiana chini ya 'Sexual Offences Special Provisions Act, 1998 ambao walifanya makosa dhidi ya watoto kama vile kubaka, kunajisi na kulawiti," ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Taarifa imefafanua kuwa msamaha huo wa rais hauwahusu wafungwa waliohukumiwa kwa makosa ya wizi wa magari kwa kutumia silaha, waliowapa mimba wanafunzi wa shule za msingi.

Pia msamaha huo, hauwahusu wafungwa waliopatikana na hatia katika makosa yanayohusu uharibifu wa miundombinu, ikiwemo wizi wa nyaya za simu na umeme, njia za reli na transfoma na wafungwa ambao wanatumikia kifungo cha pili au zaidi.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo msamaha pia hauwahusu wafungwa waliowahi kupunguziwa kifugo kwa msamaha wa rais na bado wanaendelea kutumikia sehemu ya kifugo kilichobaki, wafungwa waliohukumiwa chini ya sheria ya bodi ya Parole ya mwaka 1994, sheria ya huduma kwa Jamii ya mwaka 2002, na wafungwa waliowahi kutoroka au kujaribu kutoroka chini ya ulinzi.

Pamoja na msamaha huo wa wafungwa rais Kikwete jana alikagua gwaride la vikosi vyote vya ulinzi na usalama katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam ambako sherehe hizo, zilifanyika.

Mbali na Gwaride hilo, vijana 1000 wa shule za msingi na sekondari kutoka Tanzania na Zanzibar, nao walionyesha umahiri wao kwa kujikusanya na kutengeneza neno la 'Uhuru wa miaka 48'.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
News Archive

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©