JUMUIA YA AFRIKA MASHARIKI
KUFUNGWA MPAKA MWAKANI
14/12/2009

Jumuia
ya Afrika ya Mashariki (EAC) katika mwaka ujao itakabiliwa na changamoto
kubwa za kuhakikisha inaondoa kero wakati wa kuanza kwa Umoja kamili wa
Forodha na pia kuhakikisha nchi wanachama zina ridhia kwa wakati muafaka
itifaki ya kuanzishwa kwa soko la pamoja.
Hayo
yamebainishwa na katibu mkuu wa jumuia ya Afrika ya mashariki Balozi
Juma Mwapachu wakati wa salamu zake za kuuaga mwaka huu wa 2009 kupitia
vyombo vya habari ambapo jumuia hiyo imefunga shughuli zake mpaka mwezi
Januari Mwakani.
Balozi
Mwapachu alisema kwa Marais Jakaya Kikwete (Tanzania) Yoweri Museven
(Uganda), Mwai Kibaki (Kenya), Paul Kagame (Rwanda) na Pierre Nkurunziza
(Burundi) kusaini itifaki wa Soko la pamoja mwezi uliopita sasa itakuwa
kazi ya mabunge ya nchi hizo kuridhia itifaki hiyo.
Alisema
kuwa utekelezaji wa soko la pamoja unatakiwa kuanza kwa kasi katika
kuelekea kwenye hatua inayofuata ya kuwa na sarafu moja ya Afrika ya
mashariki.
Aidha
Balozi Mwapachu alisema katika mwaka huo nchi hizo zitakuwa na jukumu la
kuandaa mpango mkakati wa nne wa jumuia ya Afrika ya Mashariki wa mwaka
2011 na 2016 utakaolenga katika kuandaa programu za kiuchumi,ushirikiano
wa kisiasa pamoja na sekta za kijamii.
Balozi
Mwapachu alisema umekuwa na mafanikio makubwa hasa katika katika
kupitishwa kwa sera muhimu na uboreshaji wa miundombinu. Alisema kuwa
katika sera kubwa za pamoja zilizopitishwa zilikuwa ni pamoja na
mikakati ya uboreshaji wa barabara,reli,usafiri wa maji na
anga,bandari,mawasiliano ya simu,nishati na usalama wa anga.
Balozi
Mwapachu alisema kuwa mafanikio makubwa yalipatikana katika barabara
baada ya kuzinduliwa kwa ujenzi wa barabara kati ya Arusha-Nambanga hadi
Athi River Mapema mwezi Machi na wakuu wa nchi hizo katika eneo la
Lengijave wilayani Arumeru mkoani hapa.
Alisema
barabara hiyo ni muhimu katika kuunganisha kati ya Kenya na Tanzania
mpaka Unganda na baadhi ya maeneo ya Rwanda na Burundi. Balozi Mwapachu
alitaja mradi mwingine ni wa kuunganishwa nguvu ya umeme kati ya Kenya
na Tanzania katika mpaka wa Namanga.
Mipango
mingine ni pamoja na Mradi wa Kilimo na program za maendeleo
vijijini,program za maendeleo za Bonde la ziwa Victoria. Alisema pia
katika mwaka huu kumekuwepo na kazi kubwa ya ya kuhamasisha eneo hilo
kuwa la soko la pamoja na uwekezaji ambapo mkakati huo ulikamilika kwa
nchi hizo kukamilisha mchakato na hivyo kuanza rasmi kwa umoja wa
forodha ifikapo Januari mosi mwakani.
Balozi
Mwapachu alitumia fursa hiyo kuwashukuru wakuu wa nchi zote tano
zinazounda jumuia hiyi,baraza la mawaziri pamoja na asasi zote na
taasisi za jumuia hiyo pamoja na wafanyakazi wote kwa kufanikisha
malengo ya kazi za jumuia.
Aidha
Balozi Mwapachu amewashukuru wadau wengine wa karibu ndani ya jumuia
hiyo likiwemo baraza la Biashara la Afrika ya Mashariki,wananchi panoja
na washirika wa maendeleo wa jumuia hiyo kwa kutoa misaada mbalimbali ya
hali na mali.
|