Gari la mashindano (Rally)
lauwa Watano
15/12/2009

Gari lenye namba za
usajili wa Kenya KAK 9208 aina ya Subaru namba 6 ikiendeshwa na Dharam
Pandya, lilipowasili jana baada ya mbio za kilometa 41 kabla ya
kufanyika kwa awamu ya pili ya kilometa 380 leo na kupata ajali ya kuua
watu watano na kujeruhi wengine 11 eneo la Mikese Njia Nne, Wilaya ya
Morogoro, likiwa sambamba na Gari namba 7 iliyokuwa ikiendeshwa na Samiv
Nahad ‘Shanto’ juzi.

Baadhi ya Madaktari na
Wauguzi wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro wakiendelea na kazi ya kuwatibu
baadhi ya majeruhi waliopata ajali ya kugongwa na gari la mashindano yam
bio za magari leo eneo la Mikese Njia Nne Wilaya ya Morogoro.
Watu
watano wamefariki dunia leo, kati yao wanne papo hapo, baada ya gari la
mashindano ya mbio za magari kuacha barabara na kuparamia umati wa watu
waliojipanga kando kando ya njia eneo la Mikese Njia Nne, Wilaya ya
Morogoro na kuwajehuri wengine 12 na kulazwa Hospitali ya Mkoa wa
Morogoro.
Gari hiyo yenye namba za usajili kutoka Kenya KAK 9208 aina ya Subaru
likiwa miongoni mwa magari 16 yaliyoshiriki iliandikishwa namba sita ya
katika mashindano ya mbio za umbali wa kilometa 380 yajulikayo kwa jina
la Morogoro Pathfinder Rally 2009 na iliendeshwa na Dereva Dharam Pandya (29).
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Ferdinaldi Mtui ,
alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo leo majira ya saa 4: 30 asubuhi
eneo la Mikese Njia nne kwenye barabara ya vumbi baada ya gari yenye
namba KAK 9208 aina ya Subaru lililokuwa likishiriki mashindani hayo
kuacha njia ya kuwagonga watu pemebezoni mwa njia hiyo na kusababisha
vifo wa watu wa nne papo hapo na kujeruhi wengine 12 ambao walikimbizwa
Hospitali ya Mkoa na kulazwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda hiyo wa Mkoa wa Morogoro, watu waliokufa
kwenye ajali hiyo walitambuliwa kuwa ni watoto wenye umri kati ya miaka
sita na kuendelea ambao walikuwa ni miongini mwa watu waliojitokeza
kungalia mbio hizo za magari.
Alisema ajali hiyo katika barabara ya vumbi mara baada ya kufika Mikese
Mizani , ambapo magari yayo yalitumia barabara ya kawaida na gari hilo
lilipofika eneo lenye kona liliancha njia na kuwaparamia watu na
kupinduka na hivyo kusababisha vifo hivyo na majeruhi hao.
Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda huyo, kuwa kati ya maiti hizo nne ni mmoja
ndiyo iliyotambuliwa kwa jina la Jacob Mashaka (6) ambaye ni
mwanaafunzi wa Shule ya Awali katika Kijiji cha Mikese.
Naye Ofisa wa zamu wa siku ya tukio hilo katika Hosptitali ya Mkoa wa
Morogoro, Judith Kagimbwa, alisema siku hiyo walipokea majeruhi 12
waliopata ajali wakati wa mashindano ya mbio za magari iliyotokea eneo
la Mikese, Wilaya ya Morogoro.
Kwa mujibu wa Ofisa huyo wa zamu, kwamba pamoja na kuwapokea majeruhu
hao pia walipokea miili ya watu wa nne waliofariki dunia eneo la ajali
hiyo na wakiwa katika harakati za kuwatibia majeruhi hao mmoja wao
alifariki dunia akiwa wodini majira ya saa 7:30 mchana ambaye ni Said
Mohamed (40) mtanzania mwenye asili ya kiasia.
Hata hivyo Ofisa huyo wa zamu aliwataja majeruhi 11 waliolazwa kwa
kupatiwa matibabu ni Pamera Ashumba (50), Mgema Deus (16), Mwanaidi
Rajab (21), Iddi Hamis (40), Hadija Mwarabu (28), Mwamini Said (28), Juma Abdallah (33), Alex Mussa (14) Daniel Masanja (12) na Shukuru
Roma (28) ambao baadhi yao ni wakazi wa Mikese na wengine nje ya Mikese.
Kwa mujibu wa Ofisa huyo wa zamu wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro siku
ya tikio hilo, kuwa madaktari waliendelea na kazi za kuwatibia majeruhi
hao.
Ofisa Uhusiano wa Mashindano hayo, Pankaj Valambia, alisema kuwa
kufuatia ajali hiyo , wasimamizi wa mashindano hayo waliamua kusitisha
mashindano hayo ili kushughulikia watu waliopatwa na ajali hiyo pamoja
na taratibu kwa waliofiwa na ndugu zao.
“Ni kweli ajali imetokea eneo la kona kali Mikese Njia nne na kufuatia
ajali hiyo utawala na wasimamizi wa mashindano haya wamelazimika
kuyasitisha kabisa kwa lengo la kuungana na ndugu na jamaa ambao
wamefikwa sambamba na majeruhu” alisema Ofisa Uhusiano huyo.
Hata hivyo alisema Utawala na wasimamizi wa mashindano hayo wameamua
kushirikiana na ndugu hao kwa kila hali ili kuwezesha kufanikisha
shughuli mbalimbali zinazohitajika kufuatia kutokea kwa ajali hiyo.
Mashindano hayo yaliyoanza juzi kwa mbio za kilometa 41 na jana kwa
kilometa 380 yalishirikisha magari 16 kutoka Mikoa ya Iringa, Dar es
Salaam, Arusha, Tanga na Morogoro na yalizinduliwa na Mkuu wa Wilaya ya
Morogoro, Said Mwambungu jana kwenye viwanja vya Gymkana vya Mjini
Morogoro.
|