Utafutaji wa kocha mbadala
upo njiani
20/12/2009

Zengwe la kumng'oa Marcio
Maximo linapikwa na wakati wowote kuanzia sasa kocha huyu wa taifa stars
atajikuta kibarua kimeota mbawa. Uchunguzi wa globu ya jamii umebaini
kwamba hivi sasa shirikisho la soka TFF lipo njia moja kusaka mbadala
wake na mkataba wake kusitishwa kabla ya muda wake. TFF wamepata nguvu
baada ya JK ambaye analipa mshahara wa kocha huyu kutoka Brazil kuruka
kimanga na kusisitiza yeye hamlindi wala nini na haingilii mambo ya TFF
zaidi ya kusaidia kulipa mshahara wake ambao hadi sasa hakuna anayejua
ni shi'ngapi.

|