Yanga yailaza Simba mabao
2-1
24/12/2009

Timu ya
Yanga a.k.a Watoto wa Jangwani imemkung'uta mtani wake wa jadi Simba kwa
mabao 2-1 kwenye nusu fainali za kombe la Tusker Cup. Watani wemetangaza
magoli hayo kama ni zawadi nono ya Krismas kwa wapenzi wake. Alikuwa ni
Jerry Tegete aliyeweka chuma kimiani zikiwa zimebaki dakika tatu kabla
ya muda wa dakika 120 kumalizika.

Mpaka dakika 90 kwisha, mpira ulikuwa
nguvu sawa baina ya timu zote mbili kwa kutoka droo (1-1), ndipo
zilipoongezwa dakika 30 za mwisho za kutafutwa mshindi wa kombe hilo.
Kocha wa Yanga pichani akisisitiza jambo kwa kuwashajiisha vijana wa
mjini waweke kandambili pembeni, wavae njuga za kumlisha vidonge mtani
wao wa jadi Simba.

Kocha wa Yanga Kostadic Papic, au kwa jina
lingine akijulikana kama 'Clinton'.

Kocha wa Simba Patrick Phiri.

Washabiki wa Yanga wakishangilia katika
jukwaa wakati wa mchezo huo na watani wa jadi.

Washabiki wa Simba wakishangilia katika
jukwaa wakati wa mchezo huo na watani wa jadi.

Kocha wa Yanga Kostadic Papic 'Clinton'
akiwa kabebwa na mashabiki kwa kuiwezesha timu yao kuwashinda watani wa
jadi Simba kwa mabao 2-1.
|