Mount Kilimanjaro

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

 
ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

China yazindua treni ya kwanza kwa kasi duniani

27/12/2009

Baada ya Olimpiki ya mwaka 2008, China imekuwa katika kasi ya kuimarisha miundombinu ya usafiri na njia mbalimbali za maendeleo kulingana na kasi ya uchumi wa nchi yake.

China imezindua rasmi treni yake (bullet train) ambayo inajulikana kwa jila la 'Harmony Express' inasemekana inakwenda mbio kuliko treni yoyote duniani, imepita ile ya Japan na ya France; treni hiyo ya kipekee ambayo inaunganisha miji miwili ya kisasa iliyopo China ya Guangzhou na Wuhan kwa mbio za Kilomita 350 kwa saa (217miles per hour).

Treni hiyo itasaidia kupunguza muda wa usafiri wa kutoka mji mmoja mpaka mwingine kwa masaa matatu na nusu. Safari ya miji hiyo miwili kabla ya treni hii kuanza kazi huchukua muda wa masaa 7.5 (saba na nusu), lakini sasa inachuku masaa (3) matatu.

Kazi ya treni hiyo imeanza tangu mwaka 2005 kurahisisha safari za miji miwili hiyo ikiwamo Guangzhou, ambao ni mji mmoja wapo wa kisasa na ni mji mmoja wapo kama ni kitovu cha biashara uliopo kusini mwa China karibu na Hong Kong.

Wanamamlaka wa China wamesema, treni hiyo ina uwezo wa kwenda mpaka Kilomita 394.2 kwa saa; na wameshapania kujenga barabara 42 za treni hiyo kuunganisha vitongoji na miji tofauti nchini China ifikapo mwaka 2012.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
News Archive

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©