Kifimbo cha Malkia
(Queen's Baton) chaingia Tanzania
29/12/2009

Rais wa Kamati ya Olimpiki ya Tanzania,
bwana Gulam Rashid akionekana amebeba kifimbo cha Malkia (Queen's Baton)
kilipowasili katika kiwanja cha ndege cha Dar es Salaam baada ya kutoka
Nairobi, Kenya. Kuja kwa kifimbo hicho ni ishara ya Tanzania kama ni
moja ya nchi za jumuia ya madola (Commonwealth Countries) na ni ishara
kuwa Tanzania inawakilisha michezo ya Commonwealth ambayo hutokea kila
baada ya miaka minne. Imeandaliwa michezo ya (Commonwealth Games)
kufanyika mwakani 2010 mjini New Delhi, India ambapo Tanzania pia
itashariki.
Kushoto ni mwanamichezo maarufu na Katibu
wa Kamati ya Olimpiki Tanzania, bwana Filbert Bayi na kulia ni mweka
hazina wa kamati hiyo, bwana Charles Nyange. Kifimbo kitakuwa nchini kwa
ziara ya muda wa siku mbili.
|