Mount Kilimanjaro

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

 
ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Mafuriko yaikumba Kilosa

30/12/2009

Baadhi ya vijana wa eneo la Kata ya Kasiki na Mbumi wa Mjini Kilosa, wakibeba kichwani mwao godoro kuepusha lisiloane na maji ya mafuriko kutoka mto Mkondoa yaliyotokea asubuhi ya Desemba 26, mwaka huu mjini humo kufuatia mvua zilizonyesha katika milima iliyopo Wilayani Mpwapwa na Kongwa, Mkoa wa Dodoma kuanzia wiki ya Krismas.

Ng’ombe walioletwa machinjioni kwa ajili ya kuchinjwa wakiwa wamezingirwa na maji ya mafuriko yaliyotokea asubuhi ya Desemba 26, mwaka huu mjini Kilosa.

Jengo la machinjio la Mji wa Kilosa likiwa limezingirwa na maji ya mafuriko na hivyo kusababisha ng’ombe walioletwa kwa ajili ya kuchinjwa siku hiyo ya Desemba 26, mwaka huu kushindwa kuchinjwa kutokana na eneo hilo kujaa maji.

Baadhi ya vifaa vya wakazi wa Kata ya Kasiki na Mbumi za Mjini Kilosa vikiwa vimetolewa nje ya nyumba zao ili visisombwe na maji ya mafuriko yaliyotokea Desemba 26, mwaka huu mjini humo.

Gari aina ya Fuso lenye namba T 952 ABZ likiwa na magunia ya nafaka zilizookolewa kwenye moja ya nyumba iliyokumbwa na mafuriko Desemba 26, mwaka huu likijaribu kulivuta Gari jingine lililokwama eneo la mitaa ya Kata ya Kasiki, baada ya kutitia kutokana na kujaa kwa maji Barabarani kufuatia mto Mkondoa kufurika.

Diwani wa Kata ya Kasiki katika Mji wa Kilosa, Ahamed Islam (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa, Ephrem Kalimalwendo, (kulia) kwa pamoja wakimwongoza Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Issa Machibya (nyuma kulia) kuweza kuangalia baadhi ya maeneo ya mji wa Kilosa yaliyokumbwa na mafuriko ya maji asubuhi ya Desemba 26, mwaka huu.

Mkazi wa Kata ya Mbumi akiwa kabeba mikononi Cherehani yake kuepusha isiharibiwe na maji ya mafuriko yaliyotokea asubuhi ya Desemba 26, mwaka huu mjini humo baada ya mvua kubwa zilizonyesha kwenye milima iliyopo Wilayani Mpwapwa na Kongwa, Mkoa wa Dodoma kuanzia wiki ya sikukuu ya Krismas na kusababisha mto Mkondoa kufurika.

Wakazi wa nyumba moja iliyokumbwa na mafuriko wakiwa nje ya ya nyumba yao wakitafakari jinsi ya kujiokoa pamoja na mali zao zilizokuwemo ndani kama walivyokutwa eneo hilo asubuhi ya Desemba 26, mwaka huu mjini Kilosa.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
News Archive

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©