Bilioni 7 zatengwa katika
kampeni ya FIFA World Cup 2010
31/12/2009

Mwenyekiti wa Kamati ya
Rais ya FIFA 2010 Mh. Dr. Shukuru Kawambwa akiongea na wanahabari
ofisini kwake jijini Dar kuhusu maandalizi ya kamati hiyo na kampeni ya
kuhamasisha nchi washiriki wa michuano ya Kombe la Dunia kupitia hapa
nchini ama kuweka kambi kwa ajili ya maandalizi kuelekea nchini Afrika
kusini katika michuano ya Kombe la Dunia inayotarajiwa kufanyika mwakani
nchini humo. Wengine toka kulia ni Dan Mrutu, kutoka Baraza la Biashara
na Frolence Turuka, katibu mkuu wa wizara ya Sayansi Teknolojia na Elimu
ya juu.

Rais wa TFF akifafanua jambo wakati wa
mkutano huo akiwa na viongozi wengine.
HABARI KAMILI
Jumla ya
shilingi Bilioni 7 zimetengwa kwa ajili ya kugharamia kampeni ya
kuhamasisha nchi washiriki wa michuano ya Kombe la Dunia kupitia hapa
nchini ama kuweka kambi kwa ajili ya maandalizi kuelekea nchini Afrika
kusini katika michuano ya Kombe la Dunia inayotarajiwa kufanyika mwakani
nchini humo.
Waziri wa Maendeleo ya Miundombinu, Dk Shukuru Kawamba, ambaye ni
Mwenyekiti wa Kamati ya Rais ya FIFA 2010, amesema leo pesa hiyo
itatumika kwa matangazo katika vyombo mbalimbali vya habari vya ndani na
vya kimataifa, ulinzi na kuzigharamia timu na wageni.
Dk
Kawambwa kasema televisheni za Supersport kutoka Afrika Kusini na
SunVideo kutoka Brazil ziko tayari kufanya kazi ya kutangaza mambo
mbalimbali yanayohusu Tanzania na maadalizi ya timu mbalimbali
zitakazokuwa hapa nchini. Vyombo vingine ni BBC, Dautchwelle, Al jazeera
VOA na vingine vingi.
Ameelezaa kuwa kampeni hiyo itaanza mapema wakati Timu ya Ivory Coast
itapowasili nchini Januari 2 na kucheza na timu ya taifa Taifa Stars
januari 4 na pia itacheza na timu ya Rwanda Januari 7 ambayo itawasili
hapa nchini Januari 6 kwa ajili ya mchezo huo.
Rais wa
Shirikisho la Mpira nchini Leodegar Chilla Tenga amesema tayari TFF wana
mawasiliano na nchi nyingi zilizofanikiwa kuingia kwenye Fainali za
Kombe la Dunia chini Afrika Kusini.
Tenga
kazitaja nchi walizokwisha wasiliana nazo kuwa ni pamoja na Ujerumani,
Italy, Denmark, New Zealand, Brazil, Australia, Korea Kaskazini, Japan,
Argelia na Nigeria na nchi zingine ambazo bado mazungumzo yanaendelea.
Wakati
huo huo Bodi ya Utalii (TTB) ikishirikiana na TFF wameanza kampeni ya
kuhamasisha umma wa watanzania kwenda kuiunga mkono na kuishangilia
Taifa Stars wakati wa mechi yake na Ivory Coast katika mchezo wa
kirafiki Januari 4 kwenye uwanja wa Taifa.
Katika
kampeni hii kutakuwa na mabango makubwa na madogo ya matangazo,
vipeperushi, matangazo ya redio, magazeti na televisheni pamoja na
vijarida ili kuhamasisha mashabiki kwenda kushangilia timu yao.

Aina ya bango litalotumika
katika kampeni ya TTB na TFF ya kuhamasisha umma kwenda kuishangilia
Taifa Stars itapocheza na Ivory Coast January 4, 2010 katika uwanja wa
taifa jijini Dar es Salaam.
|