Mzee Rashid Mfaume Kawawa
azikwa leo
02/01/2010


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu
cha Maombolezo wakati alipowasili nyumbani kwa Marehemu Mzee Rashid
Mfaume Kawawa kushiriki katika mazishi yake yaliyofanyika nyumbani Kwake
madale jijijni Dar es Salaam.
Mzee Rashid Mfaume Kawawa amefariki dunia siku ya Alhamisi ya tarehe 31/12/2009 katika hospitali ya Taifa ya
Muhimbili alikolazwa baada ya kupata matatizo ya kiafya. Mzee
Rashid Mfaume Kawawa alijulikana kwa jina lingine kama "simba wa vita"
alizaliwa Liwale, Dar es Salaam, mwaka 1926 ambapo baada ya kushika
nyadhifa mbalimbali alikuwa Waziri Mkuu kuanzia Januari 22, 1962 hadi
Februari 13, 1977 akifuatiwa na hayati Edward Moringe Sokoine, baadaye
aikuwa Katibu Mkuu wa CCM kabla ya kustaafu kwake.

Maafisa wa jeshi
wakiwasili kaburini tayari kwa maziko ya Mzee Rashid Mfaume Kawawa.

Maafisa wa Jeshi wakijiandaa kubeba jeneza.

JK akiongoza sala ya maiti
akiwa na viongozi wengine wakuu.

Mh. Vita Kawawa (mtoto wa
Rashid Mfaume Kawawa) akiwa amejitwisha jeneza lenye mwili wa marehemu
baba yake kuelekea kaburini.

Mkuu wa majeshi mstaafu
Jenerali George Waitara (shoto) akiwa na maafisa wa ngazi za juu msibani.

Mzee Songambele akiwa na Mheshimiwa Vita
Kawawa.

Mawaziri Wakuu wastaafu msibani.

Baadhi ya waombolezaji waliofika mazikoni.

Baadhi ya waombolezaji waliofika mazikoni.

Hema kuu likiwa na viongozi mbali mbali
waliohudhuria katika maziko hayo.

Baadhi ya waombolezaji waliofika mazikoni
kumpa heshima ya mwisho Mzee Kawawa.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akiweka mchanga kaburini wakati wa mazishi ya Mzee Rashid Mfaume Kawawa
huko Madale jijini Dar es Salaam leo.

Makamu wa Rais Dk. Ali
Mohamed Shein akiweka mchanga kaburini.

Wakuu wa vyombo vya ulinzi
na usalama wakijipanga tayari kuweka mchanga kaburini.

Heshima za mwisho za kijeshi
zilihitimishwa na mizinga 19 (kumi na tisa) wakati huo.

Heshima za mwisho za kijeshi.

Kikosi cha Buruji, kikiliza "the last
post".

Shekhe Mkuu Issa Shaaban
Simba akiongea msibani. Alisisitiza umuhimu wa historia za watu kama
Mzee Rashid Mfaume Kawawa "Simba wa Vita" kuandikwa na kuhifadhiwa ili
kuwaenzi milele.
|