Burj Khalifa lafunguliwa
rasmi
04/01/2010

JENGO refu duniani kwa sasa rasmi ni Burj
Khalifa baada ya kuzinduliwa leo kwa mbwembwe za fataki na mataa ya
kung'ara, linajidai kwa kusimama urefu wa zaidi ya mita 800 (mia nane)
kushinda jengo la Taipei 101 ambalo lilisemekana kuwa ni jengo refu
duniani kabla ya Burj Khalifa kuzinduliwa. Mengine maarufu yanayofuatia
ni Petronas Towers, Sears Tower, Empire State na Canary Wharf la London.

Anga za Dubai zikimulikwa na cheche
zinazotoka kwenye jengo la Burj Khalifa mara baada ya uzinduzi rasmi wa
jengo hilo kufunguliwa kuashiria kuwa jengo hilo ndio refu kuliko yote
duniani na vilevile kuashiria Dubai inaongoza kwa majengo ya kisasa.
Sheikh Mohammed Al Maktoum (Mtawala wa Dubai) alifungua rasmi jengo hilo
baada ya kuvuta kipazia cha ukutani na kuwatangazia umati uliokusanyika
jina la jengo hilo kuwa ni 'Burj Khalifa'. Katika ufunguzi huo, baadhi
ya waliohudhuria hapo walichukuliwa na mshangao wa muda baada ya kusikia
jina la jengo hilo ni 'Burj Khalifa' badala ya 'Burj Dubai'.

Baadhi ya wakazi wa Dubai wakipita mbele
ya jengo la 'Burj Khalifa' kabla ya usiku wa jengo hilo kufunguliwa
rasmi.

Ni rasmi, jengo refu kuliko lote duniani
kwa sasa ni Burj Khalifa ambalo lilikuwa likijulikana kama Burj Dubai
kabla ya uzinduzi wake.
|