Maombolezo ya Mzee Rashid
Mfaume Kawawa - London
05/01/2010

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania waishio UK, Ndugu Abubakar Faraji
akiweka sahihi yake. Kwa majonzi makubwa amesema jina la Simba wa Vita
halikuja hivi hivi na kwamba ni kweli Mzee Rashidi Mfaume Kawawa alikuwa
Simba wa Vita vyote vya Tanganyika na baadaye Tanzania, akisimama
kidedea katika shida na raha zote nchi ilipitia. Na kwamba endapo
Mwalimu Nyerere alikuwa wino basi Mzee Kawawa alikuwa kalamu na kwa
pamoja waliweza kuiandika historia ya kipekee ya Tanzania ambayo ni
kisiwa cha upendo, amani na utulivu kutokana sio tu na busara zao bali
pia kwa kuona mbali na kuunganisha matabaka yote.

Balozi
wa Ghana, Profesa Kwaku Danso-Boafo akiweka sahihi na kusema "Afrika
imempoteza kiongozi wa kipekee. Bwana Kawawa alikuwa kiongozi aliyetutia
hamasa wanasiasa wengi Afrika, wengi wetu tuliingia kwenye siasa kwa
kufuata nyayo zake. Alichangia kiasi kikubwa kwa ukombozi wa Afrika."

Balozi
wa Papua New Guinea, Bi Jean L Kekedo, O.B.E. akiweka sahihi yake.
Amesema "Tunatoa pole kwa kifo cha kiongozi huyu mkuu."

Balozi
wa Zambia, Profesa Royson Mukwewa akiweka sahihi yake. Yeye alimwelezea
Mzee Kawawa kama "Shujaa Mkuu wa Tanzania na Afrika aliyejitolea muhanga
kupigania ukombozi wa Bara zima." Alisema njia pekee ya kumuenzi Mzee
Kawawa ni kuendeleza yale aliyoyapigania wakati wa uhai wake.

Balozi
wa Zimbabwe, Mhe. Gabriel Machinga (Picha ya juu) amesema "Tunashukuru
kwamba Mzee Kawawa ameacha historia iliyovuka mipaka ya nchi yake na
bara zima la Afrika. Atakumbukwa sana na wengi tunamshukuru kwa kazi
aliyoifanya."

Mtoto wa mdogo wa Simba wa
Vita ambaye pia ni wajina wake, Rashidi Kawawa, akiweka sahihi kwenye
kitabu cha maombolezo. Hitma imeandaliwa siku ya Jumamosi kuomboleza
kifo cha Mzee Rashid Mfaume Kawawa.

Bendera ya Tanzania ikipepea nusu mlingoti
ubalozini London, UK.
Hitma ya Mzee Rashid Mfaume Kawawa
itafanyika Jumamosi ya tarehe 09/01/2010, St Anns Mosque, St Anns Road,
Tottenham, London, N15 5GJ, SAA 9 JIONI.

|