What a beautiful scene,
white snow on GB's green!
07/01/2010

Picha pekee ambayo imenaswa na setelaiti
ya NASA, ikionyesha UK ilivyoshika barafu nchi nzima. Wataalamu wa
kusoma halihewa wamesema kuwa, kihistoria, hali hii hutokea mara moja
kila karne (miaka 100) lakini hali ya hewa haitabiriki; kawaida ifikapo
wakati wa kipupwe, UK hushuka 'snow' baadhi ya sehemu na hushuka kwa
wakati tofauti si kwa wakati mmoja kama ilivyotokea mwaka huu hali
ambayo imesababisha nchi nzima kuwa barafu.
Pamoja na kufarijika kwa hali hiyo ambayo
hutokea mara moja katika kila karne, baadhi wameathirika kiuchumi kwa
hali isiyoweza kuzuilika. Wengine wamechukua fursa ya hali hiyo
kuifurahia mandhari nzuri iliyoletwa na hali hiyo kwa kucheza nayo na
watoto wao barabarani na vibarazani "what a beautiful scene, white snow
on GB's green".
|