Mafuriko ya Kilosa
09/01/2010

Waziri Mkuu Mizengo Pinda
(kulia) akimtambulisha Waziri wa Tamisemi, Celina Kombani (kushoto)
mbele ya waathirika wa mafuriko yaliyozikumba Kata nane za Wilaya ya
Kilosa wanaoishi katika kambi ya muda ya shule ya Msingi Kondoa, wakati
Waziri Mkuu walipowatembelea kuwapa pole waathirika hao.

Waziri wa Miundombinu, Dk
Shukuru Kawambwa (watatu kutoka kushoto) akizungumza jambo na Waziri wa
Tamisemi, Celina Kombani (wapili kutoka kushoto) kuhusiana na athari za
kibinadamu na miundombinu kabla ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
kuwahutubia waathirika wa mafuriko waliopo kwenye kambi ya muda ya shule
ya Msingi Kondoa; wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya
Miundombinu, Omary Chambo.

Pichani ni sehemu ya kambi
ya muda ya waathirika wa mafuriko Kilosa.

Pichani ni sehemu ya kambi
ya muda ya waathirika wa mafuriko Kilosa.

Wananchi wakivuka mto Mkondoa katika
mafuriko yaliyokumba mto huo Kilosa.

Daraja la reli ya kati iliyokumbwa na
madhara ya mafuriko hayo.

Barabara ya Reli ikionekana pichani
ikining'inia baada ya daraja la reli hiyo kuvunjika baada ya kukumbwa na
madhara ya mafuriko.

Waziri wa Fedha na Uchumi,
Mustafa Mkullo (kushoto) akipitia orodha ya vifaa vya misaada ya dawa za
binadamu na mingine iliyotolewa na Mkurugenzi wa Hospitali ya Regency ya
Dar es Salaam iliyowasilishwa kwa Mbunge wa Jimbo la Kilosa ikiwa ni
kuwasaidia waathirika wa mafuriko yaliyotokea mjini Kilosa kuanzia
mwishoni mwa mwaka jana.
|