Tamasha la sanaa ya
uchongaji barafu China
12/01/2010

Tamasha la uchongaji
wa barafu la kimataifa nchini China limefanyika mwanzoni mwaka huu
tarehe 05 Januari 2010 katika mji wa Harbin ambao huvutia watalii wa
kutoka nchi mbalimbali duniani. Tamasha hilo limefanyika kwa mara ya 26
nchini humo kwa kuwakilishwa na wasanii mbalimbali wa kutoka nchi
tofauti ambao wakiwakilisha ufundi wao wa uchongaji barafu wa
kushabihisha miundo na mijengo maarufu mbalimbali duniani.

Wachongaji wa barafu
wakimalizia kwa kugusiagusia mchongo wao katika maonyesho ya 26 ya
uchongaji wa barafu wa kimataifa mjini Harbin, China.

Mmoja wa wakilishi
ambao waliohudhuria katika tamasha hilo akionekana katika mavazi ya
'Mickey Mouse' wa Disney mbele ya usanii wa wachongaji wa barafu nchini
China.

Harusi 28 zilifungwa siku hiyo na mabwana
na mabibi ambao wamechagua kuoana siku hiyo katika tamasha hilo. Harusi
hiyo ilipangwa na serikali ya mji huo kwa mpango na makubaliano maalum
na Wanaharusi hao na ilihudhuriwa na wawakilishi wa kutoka serikalini.

Mmoja wa wachongaji
barafu akionekana akimalizia kazi yake kwa kugusiagusia michongo ya
mwisho. Pichani ni mchongo wa aliyekuwa kiongozi wa China bwana Mao
Zedong.

Taa zilizotiwa ndani
ya barafu na nyingine zikimulika nje kung'arisha barafu, ziliwashwa
rasmi usiku wa ufunguzi wa tamasha hilo la 26 mjini Harbin
Magaharibi-Kaskazini mwa China.

Wahudhuriaji katika tamasha hilo
wakionekana wakiingia ndani ya mfano wa jengo maarufu la 'Colosseum'
lililopo Italy.

Fataki na fash-fash zikionekana katika
anga za mji wa Harbin mara baada ya ufunguzi rasmi wa uchongaji wa
barafu wa kimataifa wa 26 uliofanyika mjini Harbin, China.
Barafu za kutengenezea michongo hiyo
huchukuliwa kutoka katika mto wa Songhua ambao upo karibu na mji wa
Harbin kila mwaka huganda barafu kubwa na nyingi ambazo zinawezesha
kufanikisha ubunifu wa wasanii wa uchongaji wa barafu.
|