Mtetemeko wateketeza Haiti
13/01/2010

Mtetemeko wa ardhi
wenye ukubwa wa nguvu 7.0 umeuteketeza Haiti nchi ambayo ipo katika
visiwa vya Caribbean, Kusini mwa Marekani ya Kaskazini. Mtetemeko huo
umesababisha maelfu ya majumba kuvunjika yakiwemo mahospitali na makazi
ya watu ambao wameachwa bila ya makazi na kadiri ya watu laki moja
wasadikiwa wamekufa baada ya mtetemeko huo kutetemesha ardhi ya Haiti
jioni mwa Jumanne ya tarehe 12/01/2010.

Mtetemeko huu
haujawahi kutokea katika nchi hiyo zaidi ya miaka 200 iliyopita
ilisabibisha nchi kuingia katika usiku wa giza baada ya nchi kukosa
umeme, simu, maji, chakula na hata matibabu ya waliokumbwa na mtetemeko
huo.

Haiti ni moja ya nchi
masikini duniani na ni nchi pekee maskini katika nchi ambazo zipo
Kaskazini mwa dunia. Pia ni nchi ambayo kihistoria inajulikana kwa
kutokuwa na utulivu wa kisiasa. Mara baada ya mtetemeko huo kutingisha
nchi hiyo, misaada mbalimbali kutoka Marekani, UK, Ufaransa, China,
Venezuela na jumuia zisizo za serikali kama Red Cross na Islamic Relief
zilitangazwa katika vyombo vya habari kuelekea Haiti kusaidia watu
waliokumbwa na mtetemeko huo.

|