Mount Kilimanjaro

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

 
ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Sherehe za miaka 46 ya Mapinduzi ya Zanzibar

14/01/2010

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Amani Abeid Karume, akikagua gwaride rasmi la vikosi vya ulinzi katika kilele cha sherehe za kutimiza miaka 46 ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kiwanja cha Gombani, Pemba, asubuhi ya tarehe 12 Januari 2010.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Amani Abeid Karume na Rais Kikwete wakipokea salamu ya Heshma ya vikosi vya Ulinzi na Usalama wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 46 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika mapema asubuhi ya tarehe 12 Januari 2010, Gombani, Pemba.

Wananchi walioshiriki katika maandamano ya kusheherekea miaka 46 ya mapinduzi Zanzibar, wakipita mbele ya Mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Amani Abeid Karume, katika kiwanja cha Gombani, Pemba.

Wananchi wakiwemo Wana CUF na CCM walijumuika kwa pamoja katika kuadhimisha kilele cha miaka 46 ya Mapinduzi ya Zanzibar kama ishara wote ni wamoja na wote wanasimama kwa umoja kwa manufaa ya Zanzibar na Tanzania nzima kwa ujumla.

Kuashiria Zanzibar sasa ni moja na hakuna tofauti za kisiasa kama ilivyo kuwa hapo awali baina ya CCM na CUF, wafuasi na wanachama wa CUF walishiriki maadhimisho hayo kwa ukamilifu.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
News Archive

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©