MADE IN MUSOMA - HUMMER
HT7 (JAMVI)
16/01/2010

Gari ya Kiutamaduni
iitwayo Hummer HT7, ambayo ina injini ya Suzuki imetengezewa bodi la
Jamvi kwa ukindu na kuifanya gari hiyo kuwa ni gari pekee duniani.

Gari ya Hummer HT7
imeundwa Musoma, Tanzania, na mkazi wa Musoma ambaye anaitumia kubebea
watu kama Taxi.

Fikra ya utengezaji
gari hii ni fikra mojawapo kama fikra ya kiwanda cha BMW ambacho
wahandisi wake walitengeneza gari ya BMW kwa kutumia kitambaa.

Huu ni mwanzo wa
kukuza na kuendeleza uhandisi na usanii wa aina kama hizi kwa manufaa na
uchumi wa baadaye.

Kwa kuchanganya utamaduni na teknolojia,
gari hii imeanza kwa gea namba moja na kama inavyosemekana kila safari
huanza na hatua moja, huu ni mwanzo wa kuchanganya teknolojia na
utamaduni katika masoko ya dunia bila ya kusahau na kuzingatia mambo
yote yanayohusiana na "health and safety" kama vile kibiriti kuwa
marufuku na sigara vilevile marufuku. Tutafika!
|