Mount Kilimanjaro

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

 
ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Dk. Shein atembelea Kilosa

21/01/2010

Hii ndiyo hali halisi ya Kilosa makazi mengi ya watu bado yamezingirwa na maji shughuli nyingi bado haziendi vizuri kutokana na athari za mafuriko hayo yaliosababisha hasara ya uharibifu wa mali na maisha ya watu ambapo kwa sehemu kubwa wananchi hao wanaishi kwa shida.

Baadhi ya Mitaa ya Mji wa Kilosa bado imezingirwa na maji kutokana na mafuriko yaliyoikumba wilaya hiyo na kufanya uharibifu mkubwa wa miundombinu pamoja na mali za wananchi na kupoteza maisha kwa baadhi ya wananchi.

Makamu wa Rais Dk. Ali Mohamed Shein akitoka kukagua moja kati ya mahema ambayo yatatumika kama makazi ya muda kwa wananchi wa Wilaya ya Kilosa katika eneo la Kimamba alipotembelea Wilaya hiyo kuangalia kiwango cha athari na misaada inayohitajika.

Makamu wa Rais Dk. Ali Mohamed Shein akipata maelezo ya ujenzi wa makaazi ya muda toka kwa Mkuu wa wilaya ya Kilosa Halima Dendegu katika eneo la Magomeni mjini Kilosa wakati Dk. Shein alipofanya ziara ya kuwatembelea waathirika wa mafuriko ambayo yameikumba wilaya ya Kilosa kutokana na mto Mkondoa kujaa maji ya mvua na kina chake kupungua.

Makamu wa Rais Dk Ali Mohamed Shein akiwafariji baadhi ya waathirika wa Mafuriko yaliyoikumba wilaya ya Kilosa wakati alipowatembelea katika eneo la Magomeni ambako inajengwa kambi ya muda ya kuwasitiri wananchi hao ambao kwa sasa wamehifadhiwa katika ghala la kilichokuwa kiwanda cha mazulia Kilosa.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
News Archive

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©