Mount Kilimanjaro

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

 
ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Rais Kikwete awajulia hali majeruhi wa tukio la ujambazi

22/01/2010

Pichani Dk. Ramesh Das (shoto) akitoa maelezo ya kitabibu ya Bw. Magambo Sarali (kitandani) alipotembelewa na Rais Jakaya Kikwete. Bw. Magambo alitoa ushauri mbele ya Rais kuwa serikali inahitaji kuweka nguvu za ulinzi wa kutosha kisiwani humo kwa ajili ya usalama kwani kisiwa hicho kina kituo kimoja ambacho kipo umbali wa kilometa 20.

Inspekta Mbuma (45), majeruhi wa ajali ya msafara wa Rais iliyotokea juzi wakati Rais Kikwete akielekea mkoani Shinyanga kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo, amepigwa X ray 3 na kubainika kuwa ana uvimbe kwenye bega, amepata matibabu na kwa sasa anaendelea vizuri.

Mara baada ya Rais Kikwete kutia sahihi katika daftari la wageni, ilikuwa zamu ya Mama Salma Kikwete kama uonavyo pichani akitia sahihi.

Rais Jakaya Kikwete akiwasalimia baadhi ya Wauguzi wa Hospitali ya rufaa ya Bugando alipokwenda kuwatembelea kuwaona majeruhi wa tukio la ujambazi lililotokea katika kisiwa cha Izinga Wilayani Ukerewe, ambapo watu 13 waliuwawa hapo hapo, wakati huo huo watu 10 wakiwemo askari wawili wa Jeshi la Polisi wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kuhusika na tukio hilo la Ujambazi.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
News Archive

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©