Siku Kikwete
alipochachamaa Ikulu - Dar es Salaam
26/01/2010

Rais Jakaya
Kikwete akimuliza mmoja wa wasaidizi wake Ikulu jijini Dar es Salaam
juzi Bw. Luambiya Fyanga baada ya Rais Kikwete Kushindwa kutoa msaada wa
Magari ya wagonjwa aliyotaka kutoa kwa mkurugenzi wa mtendaji wa
Halmashauri ya wilaya ya Londigo kupokelewa na mkurugenzi mtendaji wa
Halmashauri ya Ngorongoro.
Kikwete:
''Wewe bwana unatoka wapi? alihoji Rais
Kikwete na mkurugenzi huyo aliyejitambulisha kwa jina la Kayange Jacob
alijibu ametoka wilaya ya Ngorongoro. "Unasema unatoka Ngorongoro?"
aliendelea kuhoji Rais Kikwete. "Hapa umefikaje, umekuja kufanya nini na
nani kakualika?". Aliendelea kuhoji huku akiwageukia wasaidizi wake
akiwemo Katibu wa Rais Ikulu.
"Huyu amekuja kufanya nini hapa? Nani
kamwalika", alisema Rais Kikwete ambaye sura yake ilionekana wazi
kukasirika na kulazimia kuvua miwani.
Hatuwezi kukupa gari hii. Hii ni kashfa
kubwa, nakumbuka vizuri msaada huu niliahidi kwa wananchi wa wilaya ya
Longido wakati nilipofanya ziara kijiji cha Engalinaibo kipindi cha
ukame ambapo nilifika Kituo cha Afya wakazi wa Engalinaibo wakaniambia
hawana gari la wagonjwa na nikawaahidi nitawaletea: "Nakumbuka
nilipofanya ziara wananchi wale waliniambia wanayo dispensary (Zahanati)
lakini, hawana gari la wagonjwa na sio nyinyi! Hatukupi bwana, sio lako
hatukupi."
"Hatuwezi kukupa gari, watafuteni
wanaopaswa kupewa gari hili, hii ni kashfa kubwa, document zote
zimeandikwa kwa kijiji cha Engalinaibo iweje tuwape watu wa Ngorongoro?"
alihoji.
Waombeni radhi hawa mabwana (waandishi)
mliowaalika kwa ajili ya kufanya coverage hii (kuandika habari hii) kwa
kuwasumbua, siwezi kutoa gari hapa waende tu, alisisitiza Kikwete na
kuondoka eneo la tukio kwa hasira bila kukabidhi magari hayo. Baada ya
tukio hilo Mwandishi Msaidizi wa Rais, Premi Kibanga aliwaomba radhi
waandishi wa habari kwa kuwasumbua kuhudhuria tukio hilo.
|