Uhaba wa wese Pemba
27/01/2010

Moja kati ya vituo maarufu vya kutia mafuta ya petroli
kilichopo Chake Chake kisiwani Pemba kikiwa kimevamiwa na watu na
vipando vyao kwa ajili ya kupata huduma ya kutia petroli na kufanya watu
wengi kulaza vyombo vyao. Tatizo hilo la mpito limeikumba Unguja
vilevile kwa kutoweka kwa wese kwa takriban wiki moja kufuatia
kuharibika kwa meli ya mafuta.
|