Karume atembelea utanuzi
wa bandari ya Malindi - Zanzibar
28/01/2010

Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Amani Abeid Karume,
akiwapongeza mafundi Salum Udi Mwinyi, Mhandisi wa Shirika la Bandari (kulia)
na Ali Omar, fundi wa kujitegemea, alikuwa fundi wa kampuni ya Phihi kwa
hatua ya ujenzi wa sehemu ya kuwekea makontena katika Bandari ya Malindi,
Unguja.

Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Amani Abeid Karume (kushoto)
akitoa maelekezo kwa mkurugenzi wa shirika la Bandari Zanzibar Mustafa
Aboud Jumbe wakati alipotembelea bandari ya Malindi, Unguja kuona hatua
ya maendeleo ya ujenzi wa kuongezea sehemu ya kuwekea makontena,
yanayokuja kutoka nje ya nchi, katika hatua za kuongezeka kwa uchumi wa
nchi yetu.

Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Amani Abeid Karume (katikati)
alipotembelea maendeleo ya ujenzi sehemu ya kuwekea makontena katika
Bandari ya Malindi Unguja, akifuatana na Mkurugenzi wa Shirika la
Bandari Mustafa Aboud Jumbe na viongozi wengine.
|